WOP: TUNUNUE BIDHAA ZA NDANI KUKUZA VIWANDA VYETU.

 

Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam

KATIKA kuhakikisha kunakuwepo na ustawi wa viwanda vya ndani vya bidhaa za ngozi wananchi wameshauriwa kuendelea kununua bidhaa hizo zinazozalishwa nchini ili kukuza soko la ndani.

Kwa kufanya hivyo kunaelezwa kuwa soko la ndani likiimarika ni hatua mojawapo kuendelea kukuza uchumi kuanzia kwa mfugaji na hadi kufikia kwa wazalishaji wenyewe wa bidhaa hizo zitokanazo na wanyama wanaopatikana hapa nchini.

Kenneth Woisso ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi (WOP) Woisso Original Products kilichopo Salasala jijini Dar es Salaam ambapo anasema kwa kiwango kikubwa hivi sasa soko la ndani linaonekana kufanya vizuri.

Kwa mujibu wa Woisso ni kuwa wapo baadhi ya watu ambao hupenda kukimbilia bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi ambazo hazitokani na ngozi halisi za wanyama jambo ambalo huleta hasara kwani hazidumu kwa muda mrefu

'Wapo watu ambao bado wana dhana kuwa bidhaa zikitoka nje ndizo zenye ubora kitu ambacho sio sahihi na badala yake waamini kuwa zipo bidhaa zenye ubora ambazo zinaopatikana hapa nchini kwetu' anasema

Anasema kuwa kutokana na kuingizwa kwa bidhaa zenye mfanano wa ngozi huleta hasara kwa mtumiaji kwani atalazimika kununua bidhaa hiyo mara kwa mara kwani hazitokani na ngozi halisi wakati fedha hizo angeweza kufanya jambo lingine la kimaendeleo

Hata hivyo alisema kuwa mwamko mzuri inaanza kuonekana kwa wazalishaji kuendelea kuwa wabunifu kutokana na bidhaa hizo ili kiweza kuendana na kasi ya soko ilivyo na lengo ni kushika soko la kimataifa


"Hatuwazi kuishia hapa ndani ya nchi pekee tunataka kulishika hata soko la nje kutokana na hizi bidhaa zetu tunazozalisha lengo ni kupanua wigo katika nyanja nzima ya uzalishaji wa bidhaa hizi' amasema

Mkurugenzi huyo wa WOP anasema kuwa kutokana na uzalishaji huo umeweza kutoa fursa kwa vijana mbali mbali kupata uelewa wa namna ya kutengeneza bidhaa hizo kama viatu,mikanda,mabegi,mikoba,pochi na vitu vingine vingi.


Gerald Almas ni fundi viatu ambapo anasema kuwepo wa kiwanda cha WOP mbali na kuweza kumaptia ujuzi lakini pia kinatoa fursa kwa wafanyabiashara wa sekta ya ngozi ambao kwa sasa wana uhakika wa soko la bidhaa hiyo.

"Nimepata uelewa lakini pia zipo fursa kibao zitokanazo na kuwepo wa WOP kwani hata wafanyabiashara wa ngozi sasa naonwana uhakika wa ngozi kwani mteja yupi hivyo hakuna haja ya kwenda kwenye masoko ya nje tena'anasema

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments