Na Mwandishi Wetu , Rombo
SEKTA binafsi kwa sasa zimeonekana kujikita katika kuboresha makazi ya wananchi lengo likiwa ni kuwakwamua na makazi duni kwa kurahisisha upatikanaji wa malighafi za ujenzi wa gharama nafuu
Utaratibu wa upatikanaji wa malighafi hizo kunatajwa kuwawezesha wananchi kuweza kumudu gharama za ujenzi hivyo kuwawezesha kuwa na makazi bora ya kudumu tofauti na ujenzi wa nyumba za zamani zilizojengwa kwa udongo,nyasi,au miti.
Kutokana na umuhimu huo wa makazi kampuni ya Rock Block wauzaji na wasambazaji wa matofali yatokanayo na mwamba iliyopo eneo la Holili wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro imeendelea kuhakikisha kuwa wananchi wanapata unafuu katika ujenzi kwa kupata matofali yatokanayo na miamba kwa bei rahisi ikilinganishwa na yale ya viwandani.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo Fabian Woisso amesema lengo ni kuhakikisha kuwa wananchi wanaondokana na makazi duni na badala yake wawe na makazi yaliyojengwa kwa matofali imara yanayotokana na mwamba hivyo kupunguza gharama.
'Tofali hizi zinatokana na mwamba halisi na upatikanaji wake bado ni rahisi hapa lengo ni kuhakikisha wananchi wanakuwa na nyumba imara zenye uhakika wakuhimili hata tetemeko pindi likitokea'amasema.
Anasema kuwa tofali nyingi za viwandani huwa hazina ubora kutokana na watengenezaji kutaka faida kwa kupunguza kiwango cha saruji jambo linalopelekea tofali kushindwa kuishi kwa kipindi kirefu ikilinganishwa na hizo zitokanazo na mwamba.
Mkurugenzi huyo anasema kuwa kutokana na uimara wa tofali hizo ni kuwa haziwezi kuathiriwa na fangasi au magadi kama zilivyo za kiwandani jambo linalompunguzia gharama mteja na kuwa na uhakika wa nyumba yake aliyoijenga.
"Hapa utaweza kuona kuwa wateja Wetu wakubwa ni kama shule,taasisi za dini na mashirika au kampuni mbali mbali hivyo kwa watu binafsi bado tunawahitaji sana ili kutokomeza mazingira duni'anasema.
Woisso anasema kampuni hiyo kwa sasa imekuwa ikifikisha huduma zake hizo katika mikoa ya kanda ya kaskazini ikiwemo Arusha,Tanga,Manyara na Kilimanjaro huku kukiwa na utayari kwa mteja kupata huduma hiyo kwa mkoa wowote ule.
Gadna Mshiu ni fundi ujenzi eneo la mji mdogo wa Himo ambapo anasema uimara wa malighafi hizo ikiwemo tofali na urembo mwingine umepelekea wananchi kuchangamkia ujenzi kutokana na urahisi katika upatikanaji na ni rahisi katika ujenzi.
'Hazina gharama kubwa ya sementi kwani zimenyooka hivyo matumizi ya plasta huwa kidogo tofauti na nyingine ambazo unakuta zimepinda hivyo hutumia muda na gharama ili kunyoosha'anasema
Mwisho.
![]() |






0 Comments