TINAH CHENGE AHOJI UKARABATI WA GEREZA LA BARIADI, BUNGENI.

 


Na Mwandishi wetu, Dodoma.

SERIKALI kupitia Wizara Mambo ya ndani, imesema itahakikisha inakarabati na kujenga majengo ya Magereza nchi nzima ili kuhakikisha Mazingira ya Magereza hayo yanaakisi hali ya sasa lakini pia hali ya ubinadamu. 

Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani, Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tinah Chenge aliyetaka kujua Mpango wa serikali kukarabati majengo ya Gereza la Bariadi hususani jengo la Mahabusu ambalo liko kwenye Mazingira hatarishi?.."

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tinah Chenge akiuliza swali Bungeni.

Naibu Waziri huyo alijibu, Nimshukuru sana Mheshimiwa Tinah Chenge, Mbunge wa Viti Maalumu Kwa swali lake la msingi, kama ambavyo tumetoa majibu ya awali, Serikali Ina Mpango ukarabati na ujenzi wa majengo ya Magereza nchi nzima ili kuhakikisha Mazingira ya Magereza hayo yanaakisi hali ya sasa lakini pia hali ya ubinadamu kwenye magereza tuliyorithi, na kazi hiyo tutaifanya kadri na upatiya fedha.


Mwisho.

Naibu Waziri wa Mambo ya ndani, Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud, akijibu swali Bungeni.


Post a Comment

0 Comments