Festo Shemu Kiswaga.
Na Mwandishi wetu.
ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, Festo Kiswaga, amechukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya kupitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge wa Jimbo la Ismani, Mkoani Iringa.
Zoezi hilo limefanyika katika ofisi za CCM wilaya ya Iringa vijijini, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa Chama hicho kuelekea Uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo.
Kiswaga ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi mbalimbali serikali, ni miongoni mwa wanachama waliojitokeza kuchukua fomu kuziba nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Isman, Williamu Lukuvi aliyewahi kuwa Waziri wa nchi, ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, ajira na wenye ulemavu)

0 Comments