Na Mwandishi wetu, Itilima.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, imetoa mkopo wa pikipiki 11 (kumi moja ) na Guta 1 (moja) vyenye thamani ya shilingi Mil. 40,300,000 /= kupitia mapato ya ndani.
Mikopo hiyo imetolewa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi kujiinua kiuchumi huku wanufaika wakitakiwa kurejesha fedha hizo kwa wakati ili wananchi wengine waweze kunufaika .
Akizungumza mara baada ya kukabidhi mikopo hiyo, Mkuu wa Wilaya Itilima, Anna Gidarya aliipongeza Halmashauri hiyo kwa kutenga kupitia mapato ya ndani Kwa ajili ya kuwakopesha wananchi.
Gidarya aliwataka wanufaika kutunza vifaa hivyo ili viweze kudumu na kuwaletea tija kama adhama ya serikali kuwezesha wananchi kiuchumi.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Daud Nyalamu, aliwataka wahusika kuhakikisha wanavitunza vifaa hivyo ili viwe na tija na viweze kuwaongezea kipato na kuwainua kiuchumi kama dhima ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ya Uwezeshaji kiuchumi.
Nyalamu pia ametakiwa kuhakikisha wanarejesha mkopo huu kwa wakati ili na Wananchi wengine waweze kunufaika kupitia mikopo ya serikali.
Pia wamempongeza Mkurugenzi kwa kuendelea kutenga fedha za 10% za mkopo wa wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu.
Mwisho.






0 Comments