MKUU wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, Simon Simalenga (kushoto) akiwa amemshika mtoto ambaye anawekewa alama mara baada ya kupatiwa chanjo ya polio.
Na Mwandishi wetu.
MKUU wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, Simon Simalenga, amezindua rasmi zoezi la utoaji wa chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka 10 kimkoa.
Simalenga amezindua zoezi hilo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha katika Shule ya Msingi Somanda Wilayani Bariadi huku akiwasisitiza wazazi na walezi kuhakikisha wanapeleka watoto wao ili wakapate chanjo hiyo muhimu.
Ameitaka Jamii Mkoani Simiyu kutoa ushirikiano kwa wataalamu wa Afya ili kufanikisha utekelezwaji wa zoezi la utoaji wa chanjo hiyo.
Zaidi ya watoto 800,000 watapatiwa chanjo ya POLIO Mkoani Simiyu kuanzia Tarehe ya leo ya uzinduzi Kimkoa, 24 Machi, 2026 hadi Tarehe 27 Machi 2026 kwa awamu ya kwanza, ambapo kwa awamu ya Pili zoezi hilo litafanyika kuanzia Tarehe 7 Mei 2026, hadi 10 Mei, 2026.
Mwisho.




0 Comments