CCT WANAWAKE WAKABIDHI MAGODORO NA SABUNI GEREZA LA BARIADI.

 

Viongozi wa CCT wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu wakimkabidhi msaada wa Magodoro na sabuni, Mrakibu mwandamizi wa Magereza wilaya ya Bariadi (SSP), Yona Magage.


Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

JUMUIYA ya Kikristo Tanzania (CCT) kupitia Idara ya Wanawake wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, wameadhimisha siku ya maombi duniani kwa kutoa misaada ya kibinadamu ikiwemo magodoro na sabuni katika Gereza la Bariadi Mkoani humo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi misaada hiyo, Mwenyekiti wa Wanawake CCT wilaya ya Bariadi, Mwl. Rachael Dotto amesema kuwa misaada hiyo itasaidia wafungwa kuwapunguzia adha ya ukosefu wa mahitaji hayo.

"Tumeungana na wakristo wote ulimwenguni kwa ajili ya huduma hiyo na Mungu ataendelea kuhimidiwa na kuinuliwa" amesema.



Mchungaji Oscar Pumpya, Mwenyekiti wa CCT wilaya ya Bariadi amesema kuwa wamechagua Gereza la Bariadi Kwa sababu ni sehemu muhimu sana ya kumwona yesu na kufanya hivyo ni jambo kubwa sana ambapo wengine hawahitaji msaada lakini wafungwa na mahabusu wanahitaji msaada wa hali na Mali.

Akipokea msaada huo, Mrakibu mwandamizi wa magereza (SSP), Yona Magage amewashukuru Wana jumuiya ya CCT Kwa msaada huo ikiwemo magodoro kwani walikuwa wahitaji huku akiwaasisitizawadau wengine kujitokeza kutoa misaada.


Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ni chombo kinachowaunganisha makanisa na taasisi mbalimbali za Kikristo Tanzania ili kuleta maendeleo kamilifu na endelevu.

Inajihusisha na shughuli za kiroho na kijamii, ikiwa ni pamoja na kupongeza jitihada za serikali katika kuimarisha mshikamano na utengamano nchini.

Mwisho. 









Post a Comment

0 Comments