Na COSTANTINE MATHIAS, Sengerema.
WAKULIMA wa Pamba wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wametakiwa kuzingatia Elimu ya Ugani wanayopewa na Maafisa Kilimo ili kuongeza tija ya uzalishaji.
Akizungumzia hali ya uzalishaji wa Pamba, Afisa Kilimo wa Bodi ya Pamba wilaya ya Sengerema, Salmat Kisongo, amesema kuwa wataalamu wa Kilimo kwa kushirikiana na Maafisa Ugani wa Jenga Kesho Bora (BBT) wanashirikiana kutoa huduma za ugani katika mashamba ya wakulima.
Ameeleza kuwa kwa awamu ya kwanza, wilaya hiyo imepokea chupa 39,000 za dawa ambazo zimesambazwa kwa wakulima ili kudhibiti wadudu wanaofyonza na kushambulia vitumba vya pamba.
"Tumepata chupa 39,000 za dawa, tunawaelekeza wakulima namna sahihi ya kuchanganya na kupulizia dawa hizo...tunashirikiana na BBT kutembelea wakulima, wilaya ya Sengerema tuna BBT 7 na kata ambazo hazina BBT tunatumia Maafisa Kilimo na wakulima wawezeshaji kutoa elimu" amesma.
Amesema kila mkulima atafikiwa na viuatilifu ambavyo vinasambazwa na serikali huku akisisitiza kuwa dawa hizo zinagawiwa kila baada ya muda.
Fkiri Swagi, mkulima na mkazi kutoka Kijiji Cha Isole, kata ya Buyagu, wilayani humo anamesema baada ya kupata Elimu sahihi ya ugani ameanza kulima kisasa kwa kuzingatia kanuni Bora za kilimo cha pamba.
Amesema kwa Miaka mitano sasa analima kitaalamu, pia Maafisa ugani wanatembelea mara kwa mara huku shamba lake likitumika kama dasara la kufundishia wakulima hatua za kilimo.
Daud Kayambi, mkulima na mkazi kutoka Kijiji cha Ngoma kata ya Igalulae, wilayani Sengerema Mkoani Mwanza akipulizia shamba la pamba.Makoye Nyamiti, Mwenyekiti wa kijii Cha Isole ambaye ni mkulima wa kawaida, anasema wanapata Elimu ya kilimo kutoka kwa Mkulima kiongozi ambaye amewezeshwa na anatembelea mashamba kutoa Elimu.
Mkulima Fransis Barnay, mkazi wa kata ya Buyagu, Kijiji Cha Mulaga anaipngeza serikali kupitia Bodi ya Pamba ambao wamekuwa wakitembelea shamba lake kumpatia Elimu pamoja na pembejeo za kilimo.
Mwisho.







0 Comments