Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba anatarajia kufanya ziara ya kikazi Mkoani Simiyu kuanzia tarehe 7 hadi 8 Novemba 2026.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Said M. Mtanda wakati akitoa taarifa kwa umaa ambapo amesema Waziri Mkuu akiwa Mkoani Simiyu atafanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Polisi Mwandoya pamoja na Mkutano wa Hadhara Uwanja wa Stendi Mwanhuzi wilayani Meatu.
Mtanda ameongeza kuwa siku ya pili atafanya mkutano wa Hadhara katika viwanja vya Shule ya msingi Nyamikoma wilayani Busega huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kulaki Waziri Mkuu.
Mwisho.

0 Comments