WAZIRI MKUU AMPA KADOGOSA JUKUMU LA KUSIMAMIA UJENZI BARABARA YA BARIADI-ITILIMA-MEATU-SINGIDA. ‎


‎WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara Jimbo la kisesa.

Na COSTANTINE MATHIAS, Meatu.

‎WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba amemwagia Waziri wa Ujenzi (Masanja Kadogosa) kuharakisha upembuzi yakinifu wa Barabara ya Bariadi-Itilima-Mwandoya-Meatu mpaka Singida yenye urefu wa kilometa 273 ili iweze kuingizwa katika Bajeti ya mwaka 2027/28 kwa ajili ya kuanza Utekelezaji wa ujenzi kwa kiwango cha lami.

‎Amesema kuwa ujenzi wa Barabara hiyo ni fursa muhimu kwa ajili ya kufungua fursa za Uchumi, usafiri na usafirishaji kwa wananchi kwani serikali ya Dk. Samia Suluhu Hassan ni Sikivu.

‎Akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa polisi Mwandoya wilayani Meatu Mkoani Simiyu, Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amewaelekeza kuelekeza nguvu kwenye barabara za kiuchumi.


‎WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Said Mtanda.

‎"Nataka Barabara ya lami itoke Bariadi mpaka Singida, tunataka Barabara iwe ya lami,.nakuelekeza Waziri wa Ujenzi (Kadogosa) uko hapa nenda kawasimamie watalaam Barabara hii siyo ya Mwandoya tu, hata Mara wanaitaka...inakufikisha Makao Makuu ya nchi" amesme na kuongeza.

‎"Ni Barabara ya kiuchumi na Rais Dk Samia amesema tuwekeze nguvu kwenye barabara za kiuchumi, tunapokwenda kwenye Bajeti ijayo barabara hii iwepo."

‎Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa, amesema Barabara ya Bariadi, Itilima, Mwandoya, Meatu mpaka Singida ni muhimu sana kiuchumi kwani inaunganisha Kanda tatu ambazo ni Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati na Kanda ya kasikazini.

‎Kadogosa amewahakikishia wakazi wa Simiyu kuwa watatekeleza ujenzi wa Barabara hiyo ambapo kwa sasa wanaendelea kufanya upembuzi yakinifu ili iweze kuingizwa katika mwaka wa Bajeti ujao wa 2027/28.

‎Awali Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Musa Mbuga, aliipongeza serikali kwa kutoka fedha za kutekeleza miradi ya Maendeleo katika sekta za Elimu, Afya, Maji na Barabara.

‎Amesema kuwa wananchi wa Jimbo la kisesa wanatamani Barabara ya Bariadi, itilima, Mwandoya Meatu, mpaka Singida, ijengwe kwa kiwango cha lami ili kufungua fursa za Utalii katika Hifadhi ya Serengeti, Pori la akina la Maswa game reseve na Ngorongoro, kukuza Uchumi kwa kuuza mazao, kurahisisha usafirishaji na usafiri.

‎"Tunaomba Mji wa Mwandoya ipate angalau kilometa 10 za lami sababu katika Mkoa wa Simiyu ni Jimbo la kisesa tu halina lami,...Tunaomba kupewa kipaumbele kwenye madaraja yaliyoharibika kama Mwasengela na Mbugabanhya" Amesema Mbunge huyo.

‎Mkuu wa Simiyu, Said Mtanda amesema kuwa wamejipanga kikamilifu kusimamia miradi ya serikali ili fedha za miradi zisicheweze.

‎"Meatu ni wilaya ya Utalii, na Mkoa wa Simiyu ni mkoa wa Utalii, wana Simiyu wanataka Barabara ili kuunganisha Mkoa na mikoa jirani, Bariadi, Mwandoya, Meatu na Singida tuunganishe hadi Manyara" amesema.

‎Mwisho.





Post a Comment

0 Comments