Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
Kampuni ya Jambo Group of Companies imekabidhi Hundi ya Shilingi Mil. 100 kwa timu ya Pamba Jiji Fc ikiwa ni sehemu ya pili ya Malipo ya udhamini.
Hundi hiyo imekabidhiwa leo katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, mbele ya mlezi wa timu hiyo, Said Mtanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa huo ambaye alisema fedha hizo itawasaida kulipa vizuri wachezaji wanaodai timu na kurejesha molari ili timu iweze kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya ligi Kuu nchini.
Mtanda amesema kukabidhiwa kwa Hundi hiyo ya shilingi mil. 100, itawasaidia katika uendeshaji, na kwamba mdhamini huyo alishalipa Malipo ya awali ambayo yalitumika katika mahitaji mbalimbali ya timu na sasa ni Malipo ya pili kwa ajili ya uendeshaji pia pamoja na Malipo mengine ambayo yatalipwa kabla ya ligi kuisha.
Ameishukuru kampuni ya Jambo Group huku akiahidi timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano ya ligi kuu.
Awali Mwakilishi wa Jambo Group of Companies, Saada Almasi, alisema wamekabidhi Hundi ya Mil. 100 kama Malipo ya udhamini kwa awamu ya pili mbele ya mlezi wa Timu ya Pamba Jiji ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Said Mtanda.
Amesema fedha za udhamini huo ni sehemu ya kuijenga timu ya Pamba Jiji na kuwezesha icheze na kushiriki vizuri ligi kuu ya Tanzania bara (NBC).
Timu ya Pamba Jiji Fc kutoka jijini Mwanza imecheza mechi ya kirafiki na Timu ya Simiyu Combine katika uzinduzi wa ligi hiyo ambapo pia Mkuu wa Mkoa huo alitimiza ahadi yake ya kutoa jezi ni mipira kwa timu 14 ambazo zitashiriki mashindano hayo ya kusaka bingwa wa Mkoa.
Mwisho








0 Comments