MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge akiuliza swali Bungeni.
Na COSTANTINE MATHIAS, Dodoma.
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge ameiomba serikali kutizama upya suala la Upungufu wa Samaki katika Maziwa Makuu (Victoria na Tanganyika), jambo ambalo linakwamisha uchumi na mzunguko wa fedha kwa wananchi.
Akiuliza swali ya Nyongeza, Mbunge huyo amesema kuwa "Kuna Upungufu wa samaki katika ziwa Tanganyika na siyo Tanganyika tu, hata Ziwa Victoria, ni Nini Mkakati wa serikali kuongeza samaki (Restocking) ili kukabiliana na Upungufu wa samaki kwenye maziwa yetu haya makuu."
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Ng'wasi Kamani amesema kwamba "Upungufu huo wa Samaki tunaoupata kwa Ziwa Tanganyika si K
kwa Tanganyika bali hata Ziwa Viktoria na hiyo inaathiri wananchi wanaozunguka mikoa hiyo, na hasa wanaotegemea shughuli za Uvuvi kama shughuli Kuu kukuza kiuchumi katika familia.
Amesema kuwa, Kama Wizara tunatambua changamoto tuliyonayo na tunatambua uzito wa changamoto hii katika utekeleza au kufikia malengo yetu ya dira ya Maendeleo 2050 na tumekwisha anza kuchukua hatua mbalimbali, mojawapo ni kuendeleza na kuongeza nguvu katika kupambana Uvuvi usiozingatia Sheria sababu ndio imetufikisha kwenye Upungufu wa Rasilimali hali ambayo imetufukisha katika hali hii.
"Tunaendelea kuimarisha ushiriki wa wananchi kupitia BMU lakini kwa kuwaona zaidi kupitia Tamisemi na mwaka jana tuliongeza stocking ya vifaranga 10,000 vya samaki katika ziwa Tanganyika ikiwa ni Mbinu mojawapo ya kuongeza wingi wa samaki katika ziwa hili na tutaendeleza jitihada mbalimbali za kuendelea kuwezesha wananchi hasa vijana kuingia katika Uvuvi wa samaki Kwa vizimba na kuongeza Uchumi kupitia sekta yetu, tutaendelea hatua hizi, tutaendelea kuomba na kuwasihi wananchi watoe ushirikiano sababu kwako kwenye Rasilimali hizi ili Kudhibiti Uvuvi haramu." Amesema Kamani.
Mwisho.




0 Comments