Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
CHAMA Cha Msalaba Mwekundu (Red Cross), Mkoa wa Simiyu, chini ya Mwenyekiti wake, Sitta Tumma, imeendesha mafunzo ya huduma ya kwanza baina ya voluntia wake na askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani hapa, tarehe 08 Septemba, 2026.
Lengo la mafunzo hayo ni kujengeana uwezo wa utoaji huduma ya kwanza wakati wowote na mahala popote, kabla, wakati na baada ya mvua kubwa za El-Nino, zinazotarajiwa kutokea Oktoba, 2026.
"Tumechukuwa jukumu hili na tutaendelea kuimarisha hali ya kujitolea, chini ya Kanuni Saba zinazoongoza Red Cross duniani, ambazo ni Ubinadamu, Uadilifu, Kutokupendelea, Uhuru, Kujitolea, Umoja na Ulimwengu," imesema taarifa ya Red Cross Mkoa wa Simiyu.
Katika mafunzo hayo ya pamoja, Red Cross Mkoa wa Simiyu, ilikuwa na mwalimu Hamis Shaban Mrisho, Barnabas Charles Daud, Aziz Abeod na Isaya Mganule, walioongoza masomo katika darasa hilo muhimu la kuwajengea uwezo wa utoaji huduma ya kwanza.
Mwisho.










0 Comments