RC MTANDA AKABIDHI OFISI KWA CP HAMDUNI-MWANZA.


Mwanza,

ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mohamed Mtanda ambaye kwa sasa ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Kamishna wa Polisi Said Hamduni.

Hafla ya makabidhiano imefanyika leo 6 Septemba, 2026 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa  chama na Serikali pamoja na Watumishi wa Umma Mkoani humo.

Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Mhe. Mtanda amewashukuru viongozi  wa Chama na Serikali pamoja na  watendaji kwa upendo na ushirikiano waliomuonesha wakati wote wa uongozi wake.

"Wakuu wangu wa wilaya hawa wamenipa ushirikiano wakati wote, watendaji wote nawaomba muendelee kuiheshimisha Mwanza kwa kuwapa ushirikiano mkubwa viongozi wapya mlioletewa ili lengo la kuwaletea maendeleo wananchi libaki pale pale.” alisema Mhe. Mtanda.

Aidha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumhamishia Mkoani Simiyu.

Mwisho.
















Post a Comment

0 Comments