MAKALA; FAHAMU UMUHIMU WA MATUNDU KWENYE BISKUTI.

Biskuti yenye matundu.

‎Na Mwandishi wetu.

‎MATUNDU kwenye Biskuti siyo Urembo, ukiangalia Biskuti nyingi utakutana na matundu madogomadogo juu yake, kumbe hayajawekwa kama Urembo.

‎Matundu hayo kwenye Biskuti yanaitwa Docking Holes na yana kazi muhimu wakati wa kuoka, sababu yanasaidia mvuke kutoka ndani ya Biskuti wakati wa kuoka na hivyo huzuia Biskuti kuvimba au kutengeneza mapovu.

‎Matundu hayo husaidia Biskuti kuoka vizuri na kubaki na umbo lake huku ikisaidia kupata Ile hali ya ukunjufu (Crunchy) na ukavu na inayovunjika (Crispy) kama tunayoipenda.

‎Kwa kifupi, matundu hayo madogo yana kazi kuliko unavyofikiria.

‎mwisho.

Post a Comment

0 Comments