Na Samwel Mwanga, Mbeya.
TIMU ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imeendelea kuonyesha ushindani katika Mashindano ya SHIMISEMITA 2026 yanayoendelea jijini Mbeya, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Kalambo DC katika mchezo wa mpira wa miguu.
Katika mchezo huo uliochezwa leo Agosti 22,2026 katika Shule ya Sekondari ya Ufundi Ihunga, timu hizo zilioneshana ushindani mkali na kila upande kufanikiwa kufunga bao moja na kugawana pointi.
Katika mchezo mwingine wa mashindano hayo, timu ya mpira wa pete ya Maswa DC ilionesha kiwango bora baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 25-11 dhidi ya Mpimbwe DC iliyoko mkoa wa Katavi.
Matokeo hayo yanaifanya Maswa DC kuendelea kujenga matumaini ya kufanya vizuri katika mashindano hayo yanayoshirikisha timu kutoka halmashauri mbalimbali nchini.
Michezo hiyo yote miwili ya mpira wa miguu na mpira wa pete imefanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Ufundi Ihunga jijini Mbeya, ikiwa ni sehemu ya ratiba ya SHIMISEMITA 2026.
Mashindano hayo yanaendelea huku timu mbalimbali zikiwania kufanya vizuri na kuiwakilisha vyema halmashauri zao katika michezo inayoshirikishwa.
Mwisho.




0 Comments