Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mjini, Mhandisi Kundo Mathew akiangalia maandalizi ya ujenzi wa drifiti Calvati katika daraja la Mto Ndoba.Costantine Mathias.
SERIKALI imetoa kiasi cha Shilingi Mil. 460 kwa ajili ya kujenga Daraja la Mto Ndoba unaotenganisha kata ya Bunamhala na Isanga (mtaa wa Majahida) katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Imeelezwa kuwa awali daraja hilo lilikuwa kikwazo cha Uchumi, usafiri na usafirishaji wa mazao, pia wananchi walipoteza maisha kutokana na kusombwa na Maji nyakati za masiki na kwamba kukamilika kwake kutarahisisha shughuli za kiuchumi na usafiri.
Hayo yamebainishwa jana na Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mjini, Mhandisi Kundo Mathew wakati akiwa kwenye ziara ya kata kwa kata kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Mhandisi Kundo amesema kuwa awali daraja hilo lilikuwa limejengwa chini hali iliyokuwa inahatarisha usalama wa wananchi na kukwamisha shughuli za Uchumi.
"Serikali ya Rais Dk. Samia imetoa kiasi cha shilingi Mil. 460 kujenga Daraja la juu la Mto Ndoba ili kuwaondolea adha wananchi ya kusombwa na Maji...tuendelee kuwa na imani na serikali ya Rais Dk. Samia kwani inaendelea kutekeleza miradi ya Maendeleo.
Mhandisi Kundo ameendelea na ziara yake katika Kata ya Bunamhala ili kuwasikiliza wananchi pamoja na mambo mengine amekabidhi mabati 250 Kwa ajili ya kupaua zahanati ya mwakibolo na mifuko 150 kukamilisha ujenzi.
Aidha, Mbunge Kundo amekabidhi mabati 104 kwa ajili ya kupaua Madarasa mawili ya Mahaha Sekondari, Mabati 104 kwa ajili ya kupaua madarasa mawili Giriku A pamoja Photocopy Mashine na pampu 18 za Maji.













0 Comments