TCB YAWAITA WADAU KUZINDUA MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA IGUNGA.

Zao la Pamba.

Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

BODI ya Pamba Tanzania (TCB) inapenda kuwatangazia na kuwakaribisha wadau wote katika Uzinduzi rasmi wa Msimu wa ununuzi wa Pamba wa mwaka 2026/27 kitaifa utakaofanyika tarehe  10 mei, 2026 katika Kijiji cha Mwamashimba wilayani ya Igunga Mkoani Tabora. .

Uzinduzi huu unaashiria mwanzo rasmi wa Msimu a ununuzi wa Pamba na ni jukwaa muhimu litakalowakutanisha wadau wote wa Pamba ikijumuisha wakulima wa pamba, Wanunuzi, wawekezaji, vyama vya Ushirika, Taasisi za fedha, wadau wa Kilimo pamoja na Viongozi wa serikali kwa lengo la kuendelea kuimarisha Maendeleo ya sekta ya pamba nchini. 

Mgeni Rasmi wa sherehe za Uzinduzi wa msimu wa pamba anatarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo. 

Tukio hilo litaonyesha dhamira ya serikali ya kuendelea kuleta mageuzi katika sekta-ndogo ya Pamba kupitia kuongeza Uwekezaji, kuimarisha uzalishaji, kuongeza thamani ya zao la pamba, kuboresha upatikanaji wa Masoko pamoja na kuhamasisha matumizi ya Teknolojia za kisasa katika Kilimo kupitia Mipango mbalimbali ya mageuzi ya sekta ya Kilimo. 

Aidha, kupitia Uzinduzi huo wadau watapata fursa ya Kutathimini mafanikio na changamoto za msimu uliopita wa Pamba 2025/26.

Pia, Kuhamasisha ununuzi wa Pamba unaozingatia ushindani, haki na uwazi...Kukuza uzalishaji na utunzaji wa Usafi na ubora wa Pamba, kuimarisha ushirikiano kati ya wakulima, Wanunuzi na wanaushirika. 

Bodi ya Pamba Tanzania inawaalika wadau wote wa sekta ndogo ya Pamba pamoja wananchi kushiriki katika tukio hili muhimu la kitaifa ili kuendelea kushirikiana katika kuboresha kipato cha wakulima wa Pamba na kuongeza mchango wa sekta ya Pamba katika Uchumi wa Taifa.

Post a Comment

0 Comments