Na COSTANTINE MATHIAS, Dodoma.
SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya jamii wanaendelea kutoa Elimu na pia wataboresha Mbinu za kuwafikia wanawake na makundi Maalumu ili waweze kupata mikopo yenye riba nafuu.
Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dk. Festo Dugange wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge alitaka kufahamu Mpango wa serikali kufikisha Elimu ya mikopo yenye riba nafuu inayotolewa kwa Wanawake.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dk. Festo Dugange wakati akijibu swali Bungeni leo.
"Kwa kuwa ni sera ya serikali kuwainua Wanawake kiuchumi kupitia mikopo ya asilimia 10, Je serikali Ina Mpango Gani wa kufikisha Elimu juu ya mikopo yenye riba nafuu inayotolewa na Wizara ya maendeleo ya jamii kwa Wanawake wa vijijini wa Mkoa wa Simiyu" ameuliza Mbunge huyo.
Akijibu swali hilo, Dk. Dugange amesema, "Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi pamoja na Wizara ya maendeleo ya jamii tunafanya kazi Kwa pamoja katika maeneo ya makundi Maalumu, nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge Wizara ya Maendeleo ya jamii inaendelea kuwafikia wanawake na makundi yanayohitaji kupata mikopo hiyo kupata Elimu juu ya upatikanaji wa Mikopo yenye riba nafuu" amesema na kuongeza.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge akiuliza swali Bungeni.
"Ofisi ya Waziri Mkuu tumelichukua na tunashirikiana Wizara ya Maendeleo ili kuboresha Mbinu za kuwafikia wanawake na kujua kuna fursa za mikopo hiyo"
Mwisho.
![]() |





0 Comments