SIMIYU GIRLS WAHIMIZWA KUTUMIA VIZURI ELIMU ILI INUFAISHE JAMII.

MWENYEKITI wa Seneti ya Vyuo na Vyuo vikuu Mkoa wa Simiyu kupitia UVCCM, Daud Wambura (mwenye suti nyeusi aliyekaa katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa kidato cha sita Simiyu girls.

Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

MWENYEKITI wa Seneti ya Vyuo na Vyuo vikuu Mkoa wa Simiyu kupitia UVCCM, Daud Wambura amewataka wanafunzi na vijana wanaohitimu Elimu ya Sekondari na Vyuo kutumia vizuri Teknolojia ya Mawasiliano ikiwemo mitandao ya kijamii ili iweze kuwaletea tija katika maisha yao baada ya Masomo.

Aidha Mwenyekiti huyo amewataka wanafunzi hao kutumia bunifu zao vizuri pamoja na maarifa waliyoyapa Shule ili kuleta mageuzi ya kiuchumi na kijamii katika famili zao na Taifa kwa Ujumla.

Wambura ameyasema hayo jana wakati akiongea na wanafunzi  wanaohitimu kidato cha sita Shule ya Sekondari ya wasichana Simiyu, iliyoko Igegu wilaya ya Bariadi ambapo aliwataka kutumia vizuri Teknolojia iweze kuwa fursa, nao wawe nuru na taa ya kuonyesha mwanga Kwa wenzao.

MWENYEKITI wa Seneti ya Vyuo na Vyuo vikuu Mkoa wa Simiyu kupitia UVCCM, Daud Wambura (mwenye suti nyeusi) akizungumza na wanafunzi wa kidato cha sita Simiyu girls.

"Nimeongea na wanafunzi hapa kuwahamasisha wakatumie vizuri zana (tools) walizofundishwa shuleni, changamoto kubwa watazikuta mtaani, wawe na lugha moja ya kujifunza mtaani...baada ya kuhitimu watakutana na changamoto na maisha ya uraiani, Elimu waliyoipata ikawasaidie kubadili maisha yao katika jamii." Amesema Wambura.

Amesema kuwa serikali ya Rais Dk. Samia imetengeneza Mazingira mazuri ikiwemo ujenzi wa shule na miundombinu ya kisasa ambayo imerahisisha upatikanaji wa Elimu bila upendeleo pamoja na utoaji wa Mikopo kwa Elimu ya juu ikiwemo ufadhili wa Masomo kupitia Samia scholarship.

Wambura amewasisitiza kutumia vizuri Elimu ya darasania na kwamba baada ya Masomo wakafanye kazi kama timu ili kupata mafanikio, pia Elimu waliyopata ikawasaidie wazazi kuliko kujiingiza kwnye makundi Rika mtaani.

Ester Paul, Mwanafunzi wa Simiyu girls anayesoma mchepuo wa Pcm katika masuala ya Uhandisi ameiomba serikali kuwawezesha vifaa na mikopo wanafunzi hao ili waweze kuisaidia jamii na kuleta mageuzi kutokana na Elimu waliyoipata.

"Ombi kwa serikali ituwezeshe vifaa na mikopo ili tuweze kuisaidia jamii pindi tukiwa majumbami baada ya kutoka shule, tukiwa katika jamii tunakutana na changamoto kama za Maji, Umeme na Barabara, watusaidie vifaa ili tuweze kuisaidia jamii na kuleta mageuzi" amesema.

MWENYEKITI wa Seneti ya Vyuo na Vyuo vikuu Mkoa wa Simiyu kupitia UVCCM, Daud Wambura (mwenye suti nyeusi) akiwapa zawadi wanafunzi wa kidato cha sita Simiyu girls wanatarajia kusomea Urubani.

Ameongeza kuwa jamii bado inakumbwa na Elimu ya lishe ikiwemo magonjwa ya aniemia jambo ambalo serikali inatakiwa itoe elimu sahihi ili kuondoa mwamko duni wa lishe sababu magonjwa ya lishe yamekuwa changamoto kutokana na wazazi na walezi kukosa Elimu, sambamba na Elimu waliyopata inaweza kuleta mabadiliko katika jamii.

Awali akitoa maada, afusa Maendeleo ya jamii kata ya Sapiwi, Anagroli Mvena, amewashauri wanafunzi hao baada ya kuhitimu masomo waanzishe vikundi ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na serikali ikilenga kunufaisha vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu.

Mwisho. 















Post a Comment

0 Comments