NGAWAIYA; SERIKALI NI SIKIVU, IMETENDA HAKI KWA WAHANGA WA MATUKIO YA UCHAGUZI MKUU 2025.

 

ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kilimanjaro, Thomas Ngawaiya.

Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam

ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kilimanjaro, Thomas Ngawaiya amesema kuwa serikali imesikia kilio cha wananchi walio wengi walioathiriwa na matukio ya vurugu za kabla na baada ya uchaguzi octoba 2025.

Leo April 23, 2026 rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amepokea ripoti ya tume iliyoundwa kuchunguza matukio ya vurugu zilizojitokeza kabla na baada ya uchaguzi mkuu mwaka Jana iliyowasilishwa na mwenyekiti wake jaji mkuu mstaafu Othman Chande.

Katika mapendelezo ya tume hiyo ni pamoja na serikali kugharamikia matibabu kwa wale walioathiriwa sambamba na kiwasaidia vifaa na kufanya tahimini ya hasara zilizojitokeza ili kuweza kutoa kifuta machozi kwa walioathiriwa.

Ngawaiya amesema kuwa jambo Hilo lililopendekezwa na tume na kupokelewa na mheshimiwa rais limeonyesha kuwa serikali inawajali wananchi wake na kuwa tukip Hilo halikuwa na taswira nzuri kwa taifa.

'Kiukweli hapa serikali imesikia kilio cha wananchi wengi ila katika hili ni jambo zuri maana wapo walioathiriwa na walikuwa hawahusiki kwa namba yoyote Ile na vurugu hizo' amesema.

Amesema kuwa vurugu zile hazikuwa na jambo jema ndani yake na kuwa wapo wengine walitumia mwanya huo katika kutaenda vitendo vya kihalifu ikiwemo wizi wa mali za watu pamoja na uharibifu wa mali.

Kwa mujibu wa Ngawaiya ambaye pia amehawi kuhudumu kama mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini(2000-2005)ni kuwa na yeye ni mhanga katika vurugu hizo kwani baadhi ya mali zake zilizoharibika na nyingine kupotea.

'Mimi mwenyewe ni muathirika katika matukio yale mali zangu vikiwemo viti viliharibiwa na vingine viliibiwa sasa kama kutafanyika tahimini yakuona juu ya hasara Ile ni jambo jema' anasema.

Anaongeza kuwa hakuna haki inayotafutwa kwa njià ya vurugu kama zilivyofanyika na badala yake watu hukaa katika meza ya mazungimzo ili kupata majibu kwa kile wanachokidai au kukitafuta.

Anasema vurugu zile hasipaswi kujirudia tena na si jambo la kufumbia macho kwani haileti picha nzuri kwa taifa na hata nje ya taifa kwa ujumla wake.

Mara baada ya kupokea ripoti hiyo ya tume rais Dkt Samia Suluhu Hassan amelihutubia taifa na kusema kuwa ataunda tume itakofanya tahimini ya athari walizopata wananchi na kuona jinsi ya kuweza kuwapa kifuta machozi.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments