MACHINGA COMPLEX YANUKIA BARIADI MJINI.

 

Na COSTANTINE MATHIAS, Dodoma.

SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imepokea Ombi la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge kuhusu Ujenzi wa Machinga Complex katika Mji wa Bariadi Mkoani humo.

‎Aidha, Ujenzi wa Soko la kisasa katika Mji wa Bariadi kupitia Mradi wa TACTICs unaendelea kutekelezwa kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi ambao ni Makao Makuu ya Mkoa wa Simiyu.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge akiuliza swali Bungeni leo.


‎Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Festo Dugange wakati akijibu swali la Mbunge huyo aliyetaka kufahamu, "Kwa kuwa Mji wa Bariadi unakuwa kwa haraka sana, Je Serikali haioni umuhimu wa kujenga Machinga Complex kwa ajili ya wajasiriamali wa Mkoa wa Simiyu?."

‎Akijibu Swali hiyo, Dk. Dugange amesema "Halmashauri ya Mji wa Bariadi ni miongoni mwa Halmashauri ambazo ziko kwenye Mpango wa TACTICs na nafahamu soko la Mji wa Bariadi limeingizwa katika Mpango wa TACTICs na hatua zimeanzaa kutekelezwa na litajengwa soko la kisasa sana kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi ambayo ni Makao Makuu ya Mkoa wa  Simiyu" amesema na kuongeza.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Festo Dugange wakati akijibu swali na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge.

‎"Lakini tumepokea ombi la Mheshimiwa Mbunge la kuhitaji kujenga Machinga Complex, tutafanya tathimini na kuona uwezekano wa kufanya hivyo"

‎Mwisho.





Post a Comment

0 Comments