ALIYETOA MIMBA YA MIEZI SITA ATIWA MBARONI.

 Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao.

JESHI la Polisi mkoani Tabora, linamshikilia mwanamke mmoja (21) mkazi wa Mtaa wa Singo, Kata ya Gongoni katika Halmashauri ya Manispaa Tabora kwa tuhuma za kutoa ujauzito unaokadiriwa kuwa na umri wa miezi sita.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Richard Abwao  amethibitisha kutokea tukio hilo.

Amesema  baada ya kumeza dawa ya kutoa ujauzito huo, uchafu aliuweka kwenye kopo na kuufunga kwenye mfuko ili akautupe kwenye shimo la takataka lililo jirani na eneo hilo.

Kamanda ameongeza kuwa, mbali na mtuhumiwa huyo, pia wamemkamata mwanaume mmoja (25) msukuma, mkazi wa Kata ya Chemchem katika manispaa hiyo, aliyempatia dawa za kutolea ujauzito huo.

Ameeleza sababu ya kutoa ujauzito huo kuwa ni mwanaume aliyempa mimba hiyo kuikataa.


Mwisho 

Post a Comment

0 Comments