Ng’walu Pole, mlemavu wa miguu.
KATIKA kijiji kidogo cha Mwasilimbi, Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu, anaishi kijana wa kike, mwenye miaka 19 kwa jina la *Ng’walu Pole.*
Ng’walu ni mlemavu wa akili na viungo, hali iliyomsababishia kukosa uwezo wa kuongea, kutembea wala kujihudumia mwenyewe kama watu wengine.
Ugonjwa wa degedege kwa Ng’walu haukutibiwa kwa haraka wala kwa ufanisi, hali iliyosababisha athari za kudumu katika mfumo wake wa neva.
Matokeo yake, kijana huyu sasa ana ulemavu wa viungo na akili, hawezi kutembea wala kuelewa mambo mengi, na anahitaji msaada wa karibu kwa kila jambo la kila siku kuvalishwa, kulishwa, hata kuhamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Kwa yeyote anayeguswa na simulizi hii na angetamani kusaidia, iwe ni kwa kiti cha magurudumu, chakula, au msaada wa matibabu na familia ya Ng’walu inakukaribisha kwa mikono miwili.
Anahitaji Msaada wa Kiti Mwendo
GHARAMA YA KITI MWENDO NI SHS 250,000/=
NAMBA YA KUPOKEA MCHANGO
0780446586 ABDALLAH KAGUSA
Mwisho.




0 Comments