Aidha, amesisitiza pia utekelezaji wa amri ya kina cha chini cha mshahara.
Waziri Sangu ametoa maagizo hayo alipotembelea mradi wa ujenzi wa Daraja la Mto Chombe katika Barabara ya Kaoze – Kianda, unaotekelezwa na Kampuni ya Mselem Building and Civil Engineering Co. Ltd, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani Rukwa.
Amesema serikali imeshatoa maelekezo kuhusu utekelezaji wa amri ya kima cha chini cha mshahara.
Akizungumzia suala la usalama na afya mahali pa kazi, Waziri Sangu amemwagiza mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha anazingatia sheria ya usalama na afya mahali pa kazi ili kulinda nguvu kazi ya taifa na kuzuia ajali pamoja na madhara yanayoepukika.
Katika hatua nyingine, Waziri huyo amemsisitiza mkandarasi huyo kuhakikisha anawasilisha michango ya wafanyakazi wake kwenye Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), pamoja na michango ya WCF kwa wafanyakazi wanaostahili kisheria, ili kulinda haki na ustawi wa wafanyakazi hao.
Mwisho

0 Comments