MBOLEA ZA HAI ZALETA KICHEKO KWA WAKULIMA WA PAMBA BUNDA.

 

Naye Julius Sumuni, mkulima na mkazi wa Kijiji cha Bukole kata Kunzugu wilayani Bunda Mkoani Mara akiwaonyesha namna mbolea hai ilivyosaidia kustawisha mimea ya Pamba katika shamba lake.


Na COSTANTINE MATHIAS, Bunda.


MATUMIZI ya Mbolea za Hai (Asili) kwa wakulima wa Pamba wilaya ya Bunda Mkoani Mara, yametajwa kuwa chachu ya wakulima kupata mavuno mengi ikilinganishwa na wakulima wanaolima kienyeji. 



Aidha, matumizi ya vipimo vipya vya kupandia vya sentimita 60/30 yamechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza tija kutokana na wakulima hao kupanda kisasa. 

Silas Samson, mkulima na mkazi wa Kijiji cha Kunzugu wilayani Bunda akiongea na waandishi wa Habari za Pamba juu ya umuhimu wa kutumia mbolea hai katika zao la pamba.


Wakizungumza na waandishi wa Habari za Pamba wakulima kutoka vijiji vya Kunzugu na Bukole,  kata ya Kunzugu wilayani humo, wamesema matumizi ya mbolea hai yamerejesha rutuba ya udongo iliyokuwa imepotea pia wameongezea uzalishaji


Silas Samson, mkulima na mkazi wa Kijiji cha Kunzugu, anasema matumizi ya mbolea hai na vipimo vya 60/30 vina tija sababu alilima ekari mbili za Pamba na kupata kilo 3000.



Naye Julius Sumuni, mkulima na mkazi wa Kijiji cha Bukole, anasema katika shamba lake alitumia mbolea ya samadi na ya kupandia hali iiyofanya mimea ya Pamba kustawi na kuanza kutoa vitumba vingi.




Afisa Ugani wa Kampuni ya Alliance Ginneries kupitia Jenga Kesho Bora (BBT) Kijiji cha Bukole, Rose Paul, anasema wanaelimisha wakulima kufuata kanuni za kilimo cha pamba kupitia mashamba darasa na kwamba wameandaa lita 1,000 za mbolea hai ambazo watazigawa kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji.


Mwisho 




Post a Comment

0 Comments