ITILIMA WAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BIL. 40.4.

 

Bazara la Madiwani wakiwa kwenye Kikao.


Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima. 


BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, limepitisha Rasmu ya Mpango wa Mapendekezo  ya bajeti ya kutumia kiasi cha shilingi Bil. 40.4 kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Akisoma mapendekezo hayo leo kwenye Kikao Cha Baraza la Madiwani kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri hiyo, Afisa Mipango Halmashauri hiyo, Charles Mihayo amesema kwa mwaka 2026/2027 , Halmashauri  inakadiria kukusanya, kupokea na kutumia jumla ya shilingi bilioni 40.4.

Amesema kuwa kiasi cha shilingi Bil. 26.9 ni Ruzuku ya mishahara, Bil. 1.7 ni za Matumizi mengineyo (OC) na Bil. 2.5 ni za makusanyo ya mapato ya  Ndani na Mapato Lindwa ni kiasi cha shilingi milioni 800 na pia fedha za Ruzuku wanatarajia kupokea Kutoka Serikali kuu kiasi cha shilingi bilioni 37.9.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Itilima, Daudi Nyalamu akiongea kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Itilima, Daudi Nyalamu amewasisitiza Madiwani kutekeleza agizo la ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa kila darasa kwa shilingi milioni ishirini tu na kwenda kuwahamasisha wananchi shughuli za maendeleo kama walivyoazimia kwa pamoja .
 

Mbunge wa Jimbo la Itilima, Njalu Silanga akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.


               

Mbunge wa Jimbo la Itilima, Njalu Silanga amewapongeza watalaam wa  Halmashauri ya Itilima kwa uandaaji wa Rasimu ya Bajeti ambayo itaenda kuchochea kasi ya maendeleo Vijijini. 

Mwisho.






Post a Comment

0 Comments