MKUU wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, Simon Simalenga (katikati) akiongea na wakazi wa Mtaa wa Nkuli, kata ya Guduwi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi juu ya umuhimu wa kupeleka watoto Shule.Na Neema Reuben, Bariadi.
MKUU wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, Simon Simalenga ameendelea na ziara ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi katika mtaa wa Nkuli, Kata ya Guduwi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, huku akiwasisitiza zaidi wazazi na walezi kupeleka watoto Shule.
Amewataka wazazi na walezi kupeleka watoto wao Shule ili waweze kupata haki yao ya msingi ya Elimu kutokana na serikali kuwekeza fedha nyingi kutekeleza miradi ya Elimu.
Simalenga ameonya baadhi ya wazazi na walezi ambao wanawatumikisha watoto mashambani kipindi hiki cha msimu wa mvua pia wasitumike kuchunga Mifugo.
"Serikali ya Rais Dk. Samia inatoa fedha kwa ajili ya miradi ya Maendeleo ikiwemo sekta ya Elimu, niwaombe wananchi wa mtaa wa Nkuli, kutoa ushirikiano wa kutosha kwa serikali pindi ambapo miradi ya Maendeleo inaanzishwa katika maeneo yetu ili kuwarahisishia wataalamu wetu kutekeleza majukumu yao kwa weledi kwa Maendeleo ya kata na nchi yetu kwa ujumla." Amesema.
Mwisho.





0 Comments