CCM YAIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE PERAMIHO.




Na Mwandishi wetu.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda  katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Peramiho, kwa kupata kura 69,002 kati ya kura 79,720 sawa na asilimia 87 ya kura zilizopigwa.


Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Peramiho Exavery Luyagaza alisema kuwa kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa kifungu cha 105 kifungu kidogo cha kwanza Cha Sheria ya uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani namba 1 ya mwaka 2024 ikisomwa na pamoja na kanuni ya 58C ya kanuni za uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za mwaka 2025 na kumtangaza mgombea wa CCM DK. Lazalo Bunungu kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge Jimbo la Peramiho.



Dk.Bungungu anachukuwa nafasi hiyo kufuatia kiti hicho kuwa wazi kutokana na  kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Jenista Mhagama kufariki Dunia, ambapo vyama mbalimbali 14 vya siasa vilisimamisha wagombea wakiahidi kuwaletea wananchi maendeleo.


Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Dk. Bunungu aliwashukuru wananchi wa Peramiho kwa imani yao, akiahidi kuwa mwakilishi wa wote bila kujali itikadi zao za kisiasa. Alisisitiza kuwa atashirikiana na serikali na wadau mbalimbali kuhakikisha ahadi zote zilizotolewa wakati wa kampeni zinatekelezwa kwa vitendo.


Mwisho.




Post a Comment

0 Comments