Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
MBUNGE wa Jimbo La Meatu Salum Khamis Maarufu Jambo amesema iwapo Mvua hazitanyesha ndani ya wiki tatu zijazo ,Mji Wa Mwanhuzi Utakumbwa na Changamoto Kubwa ya ukosefu wa Maji .
Jambo ameyasema hayo jana kwenye ziara ya Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ambayo imelenga Kusikiliza kero Mbali mbali za Wananchi na Kuzipatia Ufumbuzi ambapo Mkutano Huo wa Hadhara Umefanyika katika Stendi ya Mwanhuzi na kusema Wilaya ya Meatu Ni miongoni Mwa Wilaya Nchini zenye Ukame Mkubwa na Suluhu ni Maji ya ziwa Victoria.
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amepokea Ombi la Mbunge wa jimbo La Meatu na kusema Serikali itahakikisha mradi wa maji ya ziwa Victoria Unawafikia wananchi Wa Meatu awamu ya Pilli ili kuwaondolea ya adha ya Maji ya Muda .
Mwisho.







0 Comments