
Na Mwandishi wetu.
ABIRIA zaidi ya 40 waliokuwa wakisafiri na Basi la Kampuni ya Abood lenye namba za usajili T 285 EAV lililokuwa likitokea Mkoani Dar es salaam kwenda Kagera wamenusurika kifo baada ya basi hilo kuteketea kwa moto.
Ajali hiyo imetokea leo Nov 13, 2026 Majira 11 alfajiri katika Eneo la Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kwa Mujibu wa Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na ukoaji wilaya ya Kahama SSP Stanley Luhwago amesema wamefanikiwa kuuzima moto huo.
Kutokana na tukio hilo, abiria wote waliokuwamo ndani ya basi hilo wameelezwa kunusurika, huku basi hilo likiteketea kwa moto.
Chanzo cha moto huo na thamani ya mali iliyopotea bado havijaelezwa.
Mwisho.



0 Comments