Na Mwandishi wetu, Mwz.
BODI ya Pamba Tanzania (TCB), inatarajia kutekeleza Mkakati wa uzalishaji wa mbegu za pamba kwa wingi kupitia Mpango wa Building Better Tomorrow (BBT), msimu wa 2026/2027 kwa lengo la kuwapata vijana wenye umri wa miaka 18 mpaka 35, ikiwemo Wanawake, fursa za kujihusisha na uzalishaji wa mbegu za pamba kibiashara.
Programu hii itatekelezwa Simanjiro na kilindi ambapo kila mshiriki atapewa takribani ekari 10, pamoja na pembejeo, ugani, uratibu wa uvunaji na masoko.
Programu hii inalenga kuongeza uzalishaji wa Pamba, upatikanaji wa mbegu bora, ajira kwa Vijana na matumizi Bora ya viwanda vya kuchambua Pamba.
Maombi yote yawasilishe kabla ya jumanne, 20 Oktoba 2026 kupitia,
Baruapepe: info@tcb.go.tz
Mkono au posta : Mkurugenzi Mkuu l, Bodi ya Pamba Tanzania, Pamba House, S. L. P 61 Mwanza.
Ofisi ya Kanda TCB Shinyanga.
Maombi ni bure.





0 Comments