Na Costantine Mathias, Mwanza.
BODI ya Pamba Tanzania (TCB) imesema kuwa inatarajia kusambaza tani 15,000 za mbegu za pamba katika wilaya 56 zinazolima zao hilo nchini katika msimu wa 2026/2027.
Hayo yamebainishwa juzi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Mhandisi Godwin Makori wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Kilimo cha Pamba katika msimu ujao 2026/27.
Mhandisi Makori amesema kuwa hadi sasa, tani 12,000 za mbegu ya pamba zilikuwa tayari zimesambazwa katika maeneo mbalimbali yanayozalisha Pamba nchini.
Amesema Bodi hiyo imejipanga juu ya matumizi ya mifumo ya kidijitali katika usambazaji wa mbegu na pembejeo nyingine ambayo yataongeza uwazi na uwajibikaji kwa kuwezesha ufuatiliaji wa pembejeo kuanzia zinapotolewa hadi zinapowafikia wakulima waliokusudiwa.
Amesema kuwa Mfumo huo pia unalenga kuboresha usimamizi wa usambazaji na kupunguza uwezekano wa kutokea kwa dosari katika zoezi hilo.
Mwisho.

0 Comments