Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
CHAMA cha Msalaba Mwekundu (Tanzania Red Cross) Mkoani Simiyu kimesema kuwa kinaendeleea kuwajengea uwezo wanachama wake ili waweze kukabiliana na majanga pindi yanapotokea pamoja na kuokoa maisha ya wananchi wakati wa majanga.
Aidha, chama hicho kimekuwa kikishirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Mkoa huo ili kujengewa ujuzi na uwezo mbalimbali wa kukabiliana na majanga pamoja na Uokoaji ikiwemo kuimarisha huduma za jamii.
Hayo yamebainishwa jana na Mwenyekiti mpya wa Red Cross Mkoa huo, Sitta Tuma wakati wa makabidhiano ya Ofisi na Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Joyce Nyambita ambapo amesema wamejiandaa kihudumia jamii kuelekea mvua za El-Nino ambazo zinatarajiwa kunyesha hivi karibuni.
Amesema kuwa mafunzo yao na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yanalenga kuchukua tahadhali katika majanga yoyote ambayo yatajitokea katika jamii ikiwemo mvua za El-Nino hivyo wanapaswa kuchukua hatua pamoja kutoa Elimu wa kutoa Elimu ambapo wamejipanga kimafunzo na zana ili kuihudumia jamii.
"Malengo yetu ni kusogeza huduma na kuihudumia jamii katika changamoto za maisha, katika mafunzo yetu haya tunatengeneza Elimu ambayo itamnusuru mwananchi wakati wa majanga...tumejiandaa kabla, wakati na baada ya El-Nino, tunaomba jamii itoe ushirikiano kwetu" amesema.
Amefafanua kuwa katika uongozi wake wameanza kuratibu wa uanzishwaji wa miradi midogomidogo ngazi ya wilaya ili kujiongezea vipato na kwamba kila Halmashauri ya wilaya kuna kikosi cha Redcross na kwamba kila eneo ambalo litapata changamoto, kitafikiwa na kuhudumiwa na Redcross.
Mwenyekiti anayemaliza muda wake Joyce Nyambita amesema uongozi ni kupokezana vijiti na bila kufanya kazi pamoja m, taasisi haiwezi kupata Matokeo chanya.
Amesema kuwa pamoja na kumaliza muda wa uongozi wake, lakini bado ana mchango wake Redcross ikiwemo kuendelea kuihamasisha jamii kujiandaa na majanga.
Isaya Mwinule, Mwenyekiti wa Tawi la Redcross Mji wa zamani, anasema kuwa watahakikisha wanaifikia jamii kutokana na kasi ya uongozi mpya na kwamba wameijipanga kufikia jamii kama watoa huduma ya kwanza ngazi ya jamii.
Mwisho.










0 Comments