
Na Mwandishi wetu, Meatu,
MKUU wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Said Mtanda amemtaka mkandarasi wa kampuni ya SHAREE Company Limited anayetekeleza ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu kutekeleza makubaliano ya mkataba ili ujenzi wa ofisi hiyo uweze kukamilika kwa wakati.
Mtanda ametoa agizo leo Oktoba 15, 2026 katika ziara yake ya kikazi wilayani humo, hilo kufuatia uwepo wa taarifa ya kusuasua utekelezaji wa mradi huo ambapo hadi kufikia tarehe ya leo utekelezajji wa mradi huo ulikuwa umefikia asilimia
Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya miundombinu Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Boniface William, alimueleza Mkuu wa Mkoa Mtanda kuwa utekelezaji wa mradi huo utakaogharimu zaidi ya Milioni 400 umefikia asilimia 40 ambapo muda wa utekelezaji wa mradi huo umepita kwa siku 30.
Aidha amebainisha kuwa chanzo cha kusuasua utekelezaji mradi huo ni mhandisi kukosa Fedha za kutekeleza mradi licha ya Serikali kumlipa kwa mujibu wa mkataba.
Kwa upande wake Mkandarasi anayetekeleza mradi huo, Eligius Shayo alimueleza Mkuu wa Mkoa kuwa utekelezaji wa mradi huo umeathiriwa na uhaba wa malighafi ikiwemo saruji, ugumu wa ardhi wakati wa uchimbaji.
Mwisho.



0 Comments