POLISI SIMIYU YAKAMATA WATU WATATU KWA TUHUMA ZA WIZI WA BETRI ZA CT SCAN.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Edith Swebe.

Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.

JESHI la Polisi Mkoa wa Simiyu, limefanikiwa kuwakamata watu watatu kuhusiana na tuhuma za wizi wa betri za mashine ya maalum ya mionzi (CT-SCAN) zilizoibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu (Nyaumata).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Oktoba 20, 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Edith Swebe imeeleza kuwa mahojiano ya kina yanaendelea kuhusiana na wizi wa betri hizo za mashine ya mionzi pamoja na swichi ya kubadili umeme. 

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu linatoa onyo kwa baadhi ya watu ambao wanahujumu jitihada za serikali katika kuboresha miundombinu ya huduma za afya na wale wanaojipatia kipato kwa njia isiyo halali kwa kuuza au kununua vifaa vya wizi.

Mwisho.



Post a Comment

0 Comments