NAIBU WAZIRI, MHANDISI KUNDO ASHIRIKI MKUTANO WA NAIROBI CONVENTION.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

NAIBU Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, ameshiriki katika Mkutano wa Nairobi Convention unaolenga kujadili na kuimarisha juhudi za kulinda, kusimamia na kuendeleza kwa uendelevu mazingira ya bahari na maeneo ya pwani katika ukanda wa Bahari ya Hindi Magharibi.

Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre, Jijini Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi ni Makamu wa Rais Mhe. Deogratius John Ndejembi.


Nairobi Convention ni mkataba wa kikanda unaoratibiwa chini ya Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UNEP), unaolenga kukuza ushirikiano wa nchi wanachama katika uhifadhi wa bahari, pwani na rasilimali zake, pamoja na kukabiliana na changamoto za uchafuzi wa bahari, mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mifumo ikolojia.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 wanachama wa Nairobi Convention, hivyo ushiriki wake ni muhimu katika kuimarisha uhifadhi wa mikoko, matumbawe na nyasi bahari, uvuvi endelevu, udhibiti wa uchafuzi wa bahari pamoja na kukuza matumizi endelevu ya rasilimali za bahari kupitia uchumi wa buluu.

Mkutano huo pia umekadili hatua za kikanda kuhusu masuala ya uhifadhi wa mazingira ya bahari na pwani, ikiwemo mikoko, maeneo tengefu ya baharini, ocean acidification, nyasi bahari na maandalizi ya kukabiliana na uchafuzi mkubwa wa baharini.

Mwisho.


Post a Comment

0 Comments