MTANDA, SHEMSA WASHIRIKI HAFLA YA UTIAJI SAINI LESENI ZA UTAFUTAJI MAFUTA NA GESI ASILIA.

 

Na Mwandishi wetu, Dar Es Salaam,

MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Said Mtanda pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo, Shemsa Mohamed, Jana Oktoba 28, 2026, wameshiriki hafla ya utiaji saini leseni za utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika vitalu vya Mnazi Bay North, West Songosongo, Eyasi Wembere na Lindi-Mtwara, iliyofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), jijini Dar es Salaam. 

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Makamu wa Rais, Mhe. Deogratias Ndejembi na ikumbukwe kuwa Utafiti wa Mafuta na Gesi asilia umewahi kufanyika katika Mkoa wa Simiyu wilayani Meatu katika Blonde ya Eyasi Wembere.

Hafla hiyo imewakutanisha viongozi wa Serikali, wadau wa sekta ya nishati na wawakilishi wa taasisi zinazohusika na shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini, kwa lengo la kushuhudia hatua ya utiaji saini wa leseni za vitalu vilivyotajwa.

Ushiriki wa RC Mtanda katika hafla hiyo unaonesha umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya nishati katika kusimamia shughuli za uwekezaji na utafutaji wa rasilimali za mafuta na gesi asilia kwa manufaa ya maendeleo ya taifa.

Mwisho.




Post a Comment

0 Comments