
Na Mwandishi wetu.
MKUU wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Chacha Maro ameongea Maafisa usafirishaji maarufu kama Bodaboda wa Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu Oktoba 21, 2016 katika muendelezo wa Kampeni ya Ongea na Kamanda.
Amekemea vikali vitendo vya kihalifu na uhalifu vinavyofanywa na baadhi yao kwa kujihusisha na uporaji, ubakaji pamoja wizi wa mali za abiria wao wanapokua wakiwatoa sehem moja kwenda nyingine.
Aidha, ametoa wito kwa Maafisa usatirishaji hao kundelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu, lakini pia kuwa mabalozi wazuri kwenye kulinda mali za abiria wao na kuhakikisha usalama wao kwa kuvaa kofia ngumu pamoja abiria wanaopakia kwenye vyombo vyao.
Pia amewasihi kundelea kuwasilisha kero na changamoto mbalimbali za kiulinzi na usalama zinazowakuta katika mazingira ya kazi zao kwenye vituo vya Polisi hasa kipindi hiki cha kampeni yaongea na Kamanda.
Mwisho.









0 Comments