TRA YATOA MAFUNZO YA ELIMU YA KODI KWA WAFANYABIASHARA MASWA.



Na Mwandishi wetu, Maswa.

MAMLAKA ya Mapata Tanzania (TRA)  Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu imeendesha mafunzo ya Elimu ya Kodi na masuala yanayohusiana na ulipaji wa Kodi kwa Wafanyabiashara na Wajasiliamali wilayani hapa.

Akizungumza katika Mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe,  Dkt Vicent Naano Anney amesema kuwa wafanyabiashara wengi hawatoi rist ya mashine ya  EFD  hali inayopelekea kutokuwa na kumbukumbu za  bidhaa na mauzo kwa mfanyabiashara hivyo kuwataka kuwaWazalendo katika ulipaji wa Kodi.

Aidha Mhe Anney amewataka wafanyabiashara kuwa wabunifu ili kuleta ushindani wa Bidhaa kwani sekta binafsi inamchango mkubwa katika kutekeleza Dira ya Maendeleo 2050  huku akiwataka kuwa wafuatiliaji wa mabadiliko ya sharia ya kodi ili kuepuka kuingia mgogoro na serikali

“ Hivi  vikao  vya  TRA  na  Wafanyabiashara kazi yake kuwaelimisha na kuwasaidia wafanyabiashara, sasa  wafanyabiashara  wengi  wa Tanzania wana ugonjwa mmoja  hawapendi  kutoa  risti, kwahiyo ni  muhimu kwa  wafanyabiashara  kuwa na mshine ya EFD  “ DC  Maswa Vicent  Anney

Kwa Upande wake Meneja wa  TRA Wilaya ya Maswa Kisaro Fucus amesema lengo la  kuwakutanisha wafanyabiashara hao ni kuwahimiza utoaji wa risti na matumizi sahihi ya mashine za EFDs, kuwapitisha kwenye mabadiliko ya sharia za kodi kwa mwaka wa fedha  2026/2027 pamoja na kuwakumbusha ulipaji wa Kodi ya Mapato kwa awamu ya tatu.

Amesema  kuwa tunapoelekea mwisho  wa  robo ya tatu ya mwaka wa fedha  ni vizuri wafanyabiashara wakalipa kodi yao mapema kabla  ya  Tarehe 30 mwezi  wa tisa ili kuepuka  usumbufu wa  mifumo hasa kipindi cha siku za  mwisho.

Naye mwenyekiti wa wafanyabiashara wilaya ya Maswa ndugu  John  Chagu kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake ameishukuru TRA kwa kutoa elimu ya masuala ya Kodi na kuongeza kuwa  hakuna  Taifa linalofanya maendeleo bila kulipa Kodi hivyo wafanyabiashara wawe wazalendo kwa kulipa Kodi sahihi na kwa wakati

“Hakuna Nchi yoyote Duniani inayofanya maendeleo bila kulipa Kodi, Hivyo niwasihi wafanyabiashara wenzangu tulipe kodi kwa wakati na kwa Uzalendo  amesema  John Chagu - Mwenyekiti wa wafanyabiashara "

Mwisho.







Post a Comment

0 Comments