RC SIMIYU AWAITA WANANCHI KUMPOKEA NA KUSHIRIKI ZIARA YA WAZIRI MKUU.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba.

Na Mwandishi wetu.

MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Said Mtanda amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea na kushiriki katika Mkutano ya kumsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba itakayoanza Septemba 13, 2026.

Mtanda amesema kuwa katika ziara hiyo, Waziri Mkuu atapokelewa wilaya ya Maswa na kufanya Mkutano Kijiji cha Njiapanda ya Malampaka (Jimbo la Maswa Magharibi) na kwamba siku inayofuata tarehe 14/92026 atafanya Mkutano wa Hadhara viwanja Nguzonane mjini Maswa (Jimbo la Maswa Mashariki) na baadae mchana atafanya Mkutano katika uwanja wa stendi ya Langangabili wilaya ya Itilima (Jimbo la Itilima).

MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Said Mtanda

Ameongeza kuwa, Waziri Mkuu atahitimisha ziara hiyo kwa kufanya Mkutano Sapiwi, wilaya ya Bariadi (Jimbo la Bariadi Vijijini) na baadae Mkutano mwingine wa hadhara uwanja wa Sabasaba au Uwanja wa CCM mjini Bariadi (Jimbo la Bariadi Mjini) huku akiongeza kuwa Vyombo vya Ulinzi na usalama vimejipanga kuimarisha Ulinzi na usalama katika ziara hiyo. 

Mtanda amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika mikutano kwa ajili ya kusikilizia pamoja na kuwasilisha kero na changamoto zao mbele ya Waziri Mkuu.

Sikiliza hapa chini ...



Post a Comment

0 Comments