Afisa Kilimo upande wa Maabara kutoka Bodi ya Pamba, anayesimamia Usafi na Ubora wa Pamba, Doto Ntumba (kushoto) akiwaonyesha waandishi wa habari Pamba ikiwa kwenye maabara ya usanifu wa mikono.Na Costantine Mathias, Shinyanga.
BODI YA Pamba Tanzania (TCB) kwa kushirikiana na Waandishi wa Habari za Pamba na Mazingira (TACOEJ), wametoa mafunzo ya Siku moja kwa Waandishi wa Habari kutoka Mikoa mitano ya Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Mara na Geita ili kuwajengea uelewa juu ya kuandika Kwa usahihi habari za Pamba.
Pamoja na mafunzo hayo ambayo yaliyofanyika jana August 17, 2026, Waandishi hao pia wametembelea Maabara ya Usanifu wa Pamba Kwa lengo la kujifunza namna maabara hiyo inavyofanya kazi ya kusanifu Madaraja ya Pamba.
Afisa Kilimo upande wa Maabara kutoka Bodi ya Pamba, anayesimamia Usafi na Ubora wa Pamba, Doto Ntumba amesema kuwa Tanzania ina maabara moja tu ya Usanifu na Ubora wa Pamba ambayo iko Shinyanga na pia maabara hiyo unahudumia nchi za Kenya na Uganda.
Afisa Kilimo upande wa Maabara kutoka Bodi ya Pamba, anayesimamia Usafi na Ubora wa Pamba, Doto Ntumba (kushoto) akitoa maelezo kwa Waandishi wa Habari waliotembelea maabara ya usanifu wa Pamba iliyoko mkono Shinyanga.
Amesema kuwa hali ya Usafi na ubora wa Pamba bado ni ndogo, hivyo wakulima wanatakiwa kuelimishwa ili waondokane na changamoto ya uchafuzi wa Pamba.
"Maabara ya Pamba Tanzania iko moja tu Tanzania na iko hapa Shinyanga, humu tuna maabara za aina mbili, Maabara ya Usanifu wa mikono na maabara ya usanifu wa mashine...wataalamu wetu wanapokea sampuli kutoka viwandani na kutoa madaraja ya pamba" amesema na kuongeza.
"Wakulima bado wanachafua Pamba ila wakielimika nasi tutavimba kuwakuwa na Pamba safi na tutauza kwenye soko na pambe yetu utanunuliwa kwa wingi sana, waandishi wa habari mna mchango Mkubwa kuhakikisha kuhamasisha wakulima na wadau wengine kuwajibika ili tupate Pamba safi" amesema Dotto.
Amsema Serikali kupitia Bodi ya Pamba imenunua matrekta 680 Kwa ajili ya kuwarahishisha wakulima shughuli za kilimo badala ya kutumia jembe la mkono na tumeanza kusajili wakulima katika mfumo wa kidigitali ili kuwa na kanzindata pia tumeandaa ekari 1000 za kongani za viwanda Misungwi za kuongeza thamani ya zao la pamba.
Afisa Kilimo na Uhamasishaji wa zao la Pamba, Edward Nyawile amesema kuwa waandishi wa Habari akitoa Elimu juu ya umuhimu wa waandishi wa habari kuripoti habari za Pamba.Akifunga mafunzo hayo, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kanda, Afisa Kilimo wa Bodi ya Pamba Penina Range amewataka waandishi wa Habari kuwa mabalozi wa kutoa Elimu ya Kilimo cha Pamba Kwa usahihi pia wazingatie misingi ya Uandishi wa Habari.
Mafunzo hayo yamewakutanisha waandishi wa habari kutoka mikoa inayozalisha pamba, ambapo wamepata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu uzalishaji, usafi na ubora wa pamba, sera na sheria zinazosimamia zao hilo pamoja na nafasi ya vyombo vya habari katika kuelimisha na kuhamasisha wakulima.
Afisa Kilimo wa Bodi ya Pamba Penina Range akifunga mafunzo kwa Waandishi wa Habari za pamba yaliyofanyika jengo la Bodi ya Pamba Mkoani Shinyanga.Kwa upande wake, Katibu wa TACOEJ, Sitta Tuma, amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa waandishi wa habari kwa kuwa yanawaongezea maarifa na uwezo wa kuripoti na kuandika habari zinazohusu zao la pamba kwa usahihi na weledi.
Amesema zao la pamba linalimwa katika mikoa 17 nchini, hivyo ni muhimu waandishi wa habari wanaoripoti kutoka maeneo hayo kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu sekta hiyo ili waweze kutoa taarifa zenye manufaa kwa wakulima na wadau wengine.
Amesema TACOEJ itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutumia taaluma yao kuelimisha jamii na kuchochea uzalishaji wenye tija katika zao la pamba.













0 Comments