Na COSTANTINE MATHIAS.
CHUO cha Victory Western Wing College (VIWEWICO) chenye Makao Makuu wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza, kimekuja na suluhisho la kutoa Mafunzo ya Elimu kwa Mfumo wa Masafa.
Imeleezwa kuwa chuo hiki kitaendesha Mafunzo hayo ya Elimu ngazi ya Astashada (Diploma) kwa walimu wote walioko kazini na wenye Elimu ya Ualimu ngazi ya cheti ambao watajiendeleza ndani ya Mkoa wa Simiyu na nje ya Mkoa huo.
Akizungumza na SAKAGOIBOG, Mratibu wa chuo hicho Mkoa wa Simiyu, Mwl. Mabula Mvanga amesema kuwa Chuo hicho kimepata kibali rasmi cha kusajili wa kuendesha Mafunzo ya Elimu ngazi ya Diploma kwa Walimu wote Wenye ngazi ya Cheti huku wakipewa Baraka na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Prisca Kayombo.
"Chuo cha VIWEWICO, kimepata usajili chini ya NACTVET na kupata usajili namba REG/NACTVET/1403P...ada ni nafuu sana na kwamba Udahili umeanza tangu mwezi August na utahitimishwa mwezi Septemba katika maeneo yao walimu kwa kila Kata au Kanda kwa siku zitakazopangwa, mafunzo haya ya Elimu Masafa yatakuwa yatafanyika kwa kila wiki ndani ya miaka 2 tu." ameeleza Mratibu huyo.
Mabula amewaomba walimu ambao hawana Elimu ya Diploma, kuchangamkia fursa hii adhimu kwani watapata mafunzo wakiwa kazini.
Kwa maelezo zaidi, piga simu kwa Mkuu wa Chuo ndg, EMMANUEL MADUHU (0610371326) Au Mratibu Mkuu wa Chuo Simiyu, Mwl. MABULA E. MVANGA (0781148037).
Mwisho.

0 Comments