Na Mwandishi wetu, Morogoro.
MAAFISA wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), leo August 27, 2026 wametembelea kiwanda cha 21 Century Textiles Ltd kilichopo mkoani Morogoro, kinachozalisha nguo kwa kutumia pamba inayolimwa nchini Tanzania.
Ziara hiyo imelenga kuona ubora na namna pamba ya Tanzania inavyofaa kutumika katika utengenezaji wa nguo, pamoja na kutathmini mnyororo wa thamani wa zao hilo.
Aidha, maafisa hao wamepata fursa ya kujionea hatua mbalimbali za uchakataji wa pamba hadi kuzalisha nguo, ili kubaini maeneo yanayohitaji maboresho katika uzalishaji wa malighafi.
Katika ziara hiyo, TCB pia imekusudia kufahamu changamoto zinazokikabili kiwanda hicho, hususan zinazohusiana na upatikanaji na ubora wa malighafi ya pamba kutoka kwa wakulima wa Tanzania.
Ziara hiyo inatarajiwa kusaidia kuongeza ushirikiano kati ya TCB na viwanda vya nguo, huku ikilenga kuongeza matumizi ya pamba ya Tanzania katika viwanda vya ndani na kuchochea ongezeko la thamani ya zao hilo.
Changamoto kubwa zilizobainika katika ziara hiyo ni pamoja na:
1. Viwanda (Ginery) hawachambui vizuri pamba wakati mwingine wanapitisha na takataka zinazowalazimu pamba ikifika kiwandani kwao ichambuliwe tena.
2. Ubora wa pamba yetu Tanzania siyo mzuri wakulima wanachafua sana ikiwemo kuweka maji.
3. Kodi ni nyingi sana kwenye zao la Pamba hivyo wakaiomba bodi kiwepo na ruzuku wakati wa kuingiza mitambo yao ya kutengenezea nguo.
Mwisho.







0 Comments