FFU SIMIYU WAFANYA MATENDO YA HURUMA KITUO CHA BIKIRA MARIA-LAMADI.

Na Mwandishi wetu.

KIKOSI cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Simiyu, kimefanya matendo ya kuruma kwa watoto wenye mahitaji maalum kwa kutoa vifaa mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto cha Bikira Maria Mama wa Mungu Msaada wa Daima kilichopo Kata ya Lamadi Wilaya ya Busega Mkoani humo.

Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Simiyu Mkufunzi Mkuu wa Kikosi hicho Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Amosi Lujiga amesema lengo ya matendo hayo ya majitoleo ni kurudisha kwa jamii na kuliunganisha Jeshi la Polisi na jamiii.

Aidha, amesema Jeshi la Polisi ni sehemu ya Jamii hivyo wananchi waondee hofu ya kuhofia Kikosi hicho cha Kutuliza Ghasia na amesema wananchi waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Kwa upande wa mlezi wa kituo hicho cha Bikira Maria Mama wa Mungu Msaada Daima Sister Maria Helena ametoa shukurani kwa Jeshi la Polisi kwa  matendo hayo ya majitoleo kwa kuleta mahitaji hayo muhimu kwani yamekuwa msaada mkubwa kwa watoto hao imekuwa ni faraja kwao. 

Zoezi hilo limefanyika Agusti 30, 2026 katika kituo hicho cha Bikira Maria Mama wa Mungu Msaada Daima na mara baada ya zoezi hilo walishiriki katika chakula cha pamoja na watoto hao.

Mwisho.










Post a Comment

0 Comments