DC MASWA AWATAKA ASKARI MAGEREZA KUANZA MAANDALIZI YA KUSTAAFU.

 



Na Abdallah Nsabi- Simiyu.

MKUU wa wilaya ya Maswa, Dk. Vicent Naano ametoa wito kwa askari Magereza wilaya ya Maswa kuanza maandalizi ya kustaafu mapema.

Akihutubia katika maadhimisho ya Miaka Sitini na tano( 65) ya Jeshi la magereza wilaya ya Maswa katika Hafla iliyofanyika viwanja vya magereza Maswa amesema maandalizi ya kustaafu yaanze sasa.

Amewataka Askari magereza wasinisahau sana na kuendekeza starehe zisizo za Msingi.

Ameeleza Askari awe na mbinu mbadala za kutafuta pesa ikiwa pamoja na kuwa na nidhamu katika matumizi ya pesa.

Mkuu wa wilaya ya Maswa, Dk. Vicent Naano.

Mkuu huwa ametoa Rai kwa Askari kuanza hatua za kushika viwanja kwa ajili ya kujenga nyumba za makazi na kuacha tabia za kubweteka na nyumba za kambini.


Post a Comment

0 Comments