BODI YA PAMBA, TACOEJ WATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI ZA PAMBA.

Afisa Kilimo na Uhamasishaji wa zao la Pamba, Edward Nyawile akitoa maada kwenye semina iliyokutanisha Waandishi wa Habari kutoka Mikoa ya Geita, Simiyu, Mara, Mwanza na Shinyanga.

Na COSTANTINE MATHIAS, Shinyanga.

BODI YA Pamba Tanzania (TCB) kwa kushirikiana na Waandishi wa Habari za Pamba na Mazingira (Tanzania Cotton and Environmental Journalist-TACOEJ) wametoa mafunzo ya Siku moja kwa Waandishi wa Habari kutoka Mikoa mitano ili kuwajengea uwezo wa kuandika Kwa usahihi habari za Pamba.

Semina hiyo ya siku moja kwa awamu ya kwanza imefanyika Ofisi za Bodi ya Pamba Mkoani Shinyanga na imekutanisha waandishi wa Habari kutoka Mikoa ya Mara (Bunda), Geita, Mwanza, Shinyanga na Simiyu ili waweze kutoa Elimu kwa wakulima kuhusu kanuni Bora za kilimo Cha pamba na kueleza nafasi ya wadau na serikali kuendeleza sekta ndogo ya Pamba.

‎Akizungumza wakati wa Kufungua mafunzo hayo, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Kanda ya Magharibi (Renatus Philibert), Penina Range ambaye ni Afisa Kilimo wa Bodi ya Pamba amewataka waandishi wa habari kuzingatia weledi wakati wanaripoti na kuandika habari za pamba. 

‎Penina amewataka waandishi wa habari kutumia vyombo vyao vya habari kutoa ujumbe sahihi na taarifa sahihi zinazotoka vyanzo sahihi kama Bodi ya Pamba ili wakulima waweze kujenga uelewa na kuongeza tija katika uzalishaji wa Pamba.

‎"Kupitia Mafunzo haya mkawe mabalozi wa kuelimisha wakulima ili kuongeza tija ya uzalishaji wa Pamba, wakulima wengi wanahitaji Elimu sahihi toka kwa Waandishi habari... andikeni kwa usahihi, weledi na kuzingatia taaluma zenu" amesema Penina na kuongeza.

‎"tuwe mabalozi kama unahisi unachokitoa huna usahihi nacho, tuwasiliane na Bodi ya Pamba sababu viongozi wapo na watatoa ushirikiano muda wote, tunataka kiunganishi baina yetu na wadau wa Pamba, hatuna uwezo wa kuwafikia wadau wote bila nyie".

‎Awali akiwasilisha maada kwenye semina hiyo, Afisa Kilimo na Uhamasishaji wa zao la Pamba, Edward Nyawile amesema kuwa waandishi wa Habari Wana mchango Mkubwa kwenye sekta ndogo ya Pamba na kwamba zao la pamba linasimamiwa chini ya Sheria namba 2 ya mwaka 2001.

‎Amesema Serikali kupitia Bodi ya Pamba imenunua matrekta 680 Kwa ajili ya kuwarahishisha wakulima shughuli za kilimo badala ya kutumia jembe la mkono na tumeanza kusajili wakulima katika mfumo wa kidigitali ili kuwa na kanzindata pia tumeandaa ekari 1000 za kongani za viwanda Misungwi za kuongeza thamani ya zao la pamba.

Akiwasilisha maada ya Usafi na Ubora wa Pamba, Doto Ntumba, Afisa Kilimo upande wa Maabara kutoka Bodi ya Pamba, Doto Ntumba amesema kuwa Tanzania Ina maabara moja tu ya Usanifu wa Pamba ambayo Iko Shinyanga na pia maabara hiyo unahudumia nchi za Kenya na Uganda.

‎Amesema kuwa hali ya Usafi ni ubora wa Pamba Bado ni ndogo ambapo wakulima Bado wanakabiliwa na changamoto ya uchafuzi wa Pamba.

‎"Hapa tuna maabara za aina mbili, Maabara ya Usanifu wa mikono na maabara ya usanifu wa mashine, wataalamu wetu wanapokea sampuli na kutoa madaraja ya pamba, wakulima wakielimika nasi tutavimba kuwakuwa na Pamba safi na tutauza kwenye soko na pambe yetu utanunuliwa kwa wingi sana, waandishi wa habari mna mchango Mkubwa kuhakikisha tunapata Pamba safi" amesema Dotto.

Afisa Kilimo upande wa Maabara kutoka Bodi ya Pamba, Doto Ntumba.

‎Sitta Tuma, Katibu wa TACOEJ, amesema kuwa Mafunzo hayo ni muhimu kwa Waandishi wa Habari kwa lengo la kuwaongezea uwezo wa kuripoti na kuandika habari za pamba. 

‎Amesema kuwa zao la Pamba linazalisha katika mikoa 17 nchini, hivyo ni muhimu waandishi wa habari wakapatiwa mafunzo ambayo watayatumia kuelimisha jamii ili kuchochea uzalishaji wenye tija katika zao hilo muhimu la kibiashara nchini.

Sitta Tuma, Katibu wa TACOEJ, akitoa maada kwenye semina ya Waandishi wa habari za pamba na Mazingira iliyofanyika jengo la Bodi ya Pamba Shinyanga.

Moshi Ndugulile, Mwandishi wa Habari na Mtangazaji kutoka Faraja Fm, amesema kuwa wakulima wa Pamba wanahitaji kupewa Elimu ili kurejesha uzalishaji wa Pamba kama miaka ya nyumba ambapo Pamba iliiitwa dhahabu nyeupe.

Kupitia semina hiyo, waandishi wa habari wamepata nafasi ya kutembelea maabara ya pamba na kupata Elimu namna inavyofanya kazi ya kulima ubora wa pamba na kutoa madaraja ya Pamba.

Aidha, Mafunzo hayo yamelenga kupata waandishi wa habari mahiri (champion) kupitia habari za pamba ili kuongeza hamasa na Uwajibikaji wa wadau katika Kilimo cha zao la pamba.

MWISHO.







































Post a Comment

0 Comments