MWENGE WAZINDUA MRADI WA MAJI NKOLOLO, KUNUFAISHA WAKAZI 2,097.


Mradi wa Maji katika Kijiji cha Nkololo wilayani ya Itilima Mkoani Simiyu.

Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.

MWENGE wa Uhuru umezindua Mradi wa Maji ulipo Kijiji cha Nkololo, kata ya Mwamapalala wilayani Itilima Mkoani Simiyu wenye thamani ya shilingi mil. 107 ambao utanufaisha wakazi 2,097 na kwamba umetekelezwa kupitia mradi Lipa kwa Matokeo awamu ya nne (PforR-IV).

‎Akizungumza kabla ya kuzindua Mradi huo, Kiongozi za mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2026, Michael Wazo Mwang'onda, amempongeza Rais Dk. Samia kwa kuendelea kuboresha sekta ya Maji kwani wakati anaingia madarakani aliwaahidi wakina mama kuwatua ndoo kichwani.

‎"Tumashukuru Rais Dk. Samia kutekeleza mradi wa upanuzi wa huduma Maji kwa wananchi...huduma hii inapatikana Kwa wananchi 20,97, Mwenge wa Uhuru umekagua na tumeona katika mikoa yote tuliyopita, maji yanakwenda na leo hapa Nkololo zaidi ya shilingi mil. 100 zimeletwa ili wananchi wapate maji karibu na maeneo yao" amesema kiongozi huyo.

Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa 2026, Wazo Mwang'onda (kulia) akizindua Mradi wa Maji katika Kijiji cha Nkololo wilayani Itilima, kushoto Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Simiyu, wengine ni Katibu wa CCM wilaya ya Itilima Joel Makwaiya pamoja na kuu wa Wilaya hiyo, Anna Gidarya.

‎Mwang'onda amewasisitiza wananchi juu ya umuhimu wa kulinda amani ili serikali iweze kuleta Maendeleo makubwa zaidi ya haya ambayo wanayaona huku akiwasisitiza kutunza miundombinu ya Maji ili endelevu.

‎Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa Mradi, Meneja wa Wakala ya Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA), wilaya ya Itilima, Mhandisi Yahya Husein, amesema Mradi huo imehusisha ujenzi wa vioski vitano kwenye Vijiji vya Gambasingu, Nkololo, Mwaogama, Manhunda na Mwaswale pamoja na uwekaji wa Simtanki tano zenye ujazo wa Lita 10,000 kila Kijiji.

Meneja wa Wakala ya Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA), wilaya ya Itilima, Mhandisi Yahya Husein, akitoa taarifa ya ujenzi wa Mradi wa Maji katika Nkololo mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge (hayupo pichani).

‎"Mradi huu umegharimu shilingi Mil. 107, fedha zote zinatoka serikali Kuu kupitia program ya lipa kwa Matokeo awamu ya nne (pforR-IV), unahudumia wakazi 2,907 wa Kijiji cha Nkololo na umepunguza umbali na muda wa wananchi hasa akina mama kutafuta Maji" amesema.

‎Mbunge wa Jimbo la Itilima, Njalu Silanga amesema serikali ya Rais Dk. Samia inaendelea kuleta Maendeleo katika sekta za Maji, Umeme, Barabara na Elimu na kwamba kupitia mradi huo wa Maji, zaidi ya wananchi 2000 watanufaika.

Mbunge wa Jimbo la Itilima, Njalu Silanga (kulia) akisalimia na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2026, Wazo Mwang'onda.

‎Masunga Simon, mkazi wa Kijiji cha Nkololo amesema kabla ya Mradi huo wa Maji, wananchi hao walikuwa wanapata Maji kwa kulowa kwenye visima ambapo Maji yake siyo safi na salama.

‎Makoye Lubonya, mkazi wa Nkololo ameishukuru serikali kwa kuwaletea Mradi wa Maji karibu na makazi yao na kuongeza kuwa kabla ya Mradi huo,wakina mama walikuwa wanahangaika kusaka Maji umbali mrefu.

‎Naye Sita Nkiliti amesema kuwa kabla ya Mradi huo wananchi walikuwa wanafuata Maji mto Simiyu, Maji ambayo siyo safi na salama, hivyo wanashukuru kupata Maji ambayo ni salama.

‎Helena Edward, mkazi wa Nkololo amesema kabla ya Mradi huo walikuwa tunapata shida ya Maji, tulikuwa tunakunywa Maji machafu, Bomba lilikuwa ni moja, tunafurahu Ruwasa kutuletea Maji karibu na makazi yetu.

‎Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijni (RUWASA), Mkoa wa Simiyu, Mhandisi  Emmanuel Luswetula amesema kuwa wametekeleza Mradi huo  kulingana na mahitaji, wananchi kwani awali hawakua na maji ya uhakika.

‎Amesema kuwa mradi huo ni suluhisho la changamoto ya Maji, na wataendelea kusogeza huduma ya Maji ambapo mpaka sasa upatikanaji wa Maji katika Mkoa wa Simiyu umefikia asilimia 71.


‎Mhandisi Luswetula amesema kuwa serikali inawekeza fedha nyingi katika miradi ya Maji ambapo aliwasisitiza wananchi kutunza  Miradi hiyo ili iwe endelevu.

‎Mwisho.













Post a Comment

0 Comments