MRADI WA MAJI IHUSI KUNUFAISHA WAKAZI 16,000.

                      Tenki la Mradi wa Maji Ihusi.

‎Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

‎KUKAMILIKA kwa Ujenzi wa Mradi wa Maji Ihusi ambao utahudumia vijiji vya Ihusi, Mwasilimbi na Mwashagata wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, umelenga kuwaondolea adha ya kutafuta Maji umbali mrefu wakazi zaidi ya 16,000.

‎Imeelezwa kuwa tangu Uhuru, vijiji hivyo havijawahi kupata Maji safi na salama na badala yake wananchi walikuwa wanatumia Maji ya kwenye Malambo ambayo walikuwa wanachangia na Mifugo pia hayakuwa safi na salama.

‎Akisoma taarifa ya Ujenzi wa Mradi huo, Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) wilaya ya Bariadi, Mhandisi Moses Mwampunga amesema kuwa ujenzi wa Mradi huo ulianza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 na kwamba hadi kukamilika utagharimu kiasi cha shilingi Bil. 1.5.

‎Amesema kuwa baada ya Mradi huo kukamilika utahudumia wakazi  16,713,  vituo 15 vya kuchotea Maji, na birika la kunyeshwea mifugo pia utaongeza upatikanaji wa huduma za Maji kutoka asilima 64 mwaka 2021 hadi asilima 82.1 pamoja na kuongeza idadi ya wanufaika kwa zaidi kufikia asilima 90 ifikapo 2030.

‎Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga amesema pamoja na serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kutoa fedha za kutekeleza Mradi wa mabadiliko ya taiba nchi, Bado anatoa fedha kujenga miradi ya maji ikiwemo Mradi wa Ihusi ambao ni muhimu kwa maisha na ukuaji wa Uchumi wa wananchi.


‎Akizungumza kabla ya kuweka jiwe la Msingi, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026, Wazo Mwang'onda amesema kuwa ahadi ya Rais Dk. Samia ya kuwatua ndoo akina mama unatekelezwa kwa vitendo sababu miradi inatekelezwa mpaka vijijini.

‎"Rais aliahidi anakwenda kumtua mama ndio kichwani, tunashuhudia Maji yanafika kwa wananchi iwe mjini au vijijini...Rais amedhamiria kufikisha Maji karbu na Wananchi, hataki kuona akina mama na watoto wakihangaika kutafuta Maji, akina mama ndio wanahangaika usiku na mchana kuhakikisha familia ipata Maji, wananchi wa maeneo haya wanakwenda kupata Maji karibu na makazi ya wananchi" amesema.

‎Kiongozi huyo wa Mwenge wa Uhuru 2026, amewataka wananchi kuendelea kumwombea Rais Dk. Samia pamoja na kuendelea kulinda amani ili serikali iendelee kuleta Maendeleo kama haya wanayaona.



‎Amewataka pia kutunza miundombinu ya Maji ili itumike kizazi na kizazi huku akitolea Mfano kuwa kuna na wakati miundombinu iliharibiwa na wananchi wakakosa Maji, hivyo amepatikana Rais Samia aliyedhamiria kuwasogezea huduma ya Maji, wanapaswa kutunza Miradi ya Maji.

‎Esta Mabushangila, mkazi wa kijiji cha Ihusi ameipongeza serikali kwa kutekeleza mradi huo wa Maji ambao utakuwa mwarobaini wa changamoto ya ukosefu wa maji

‎Nye Maduhu Mpemba, Mwenyekiti wa Kijiji cha Ihusi, amesema tangu Uhuru Kijiji hicho hakijawahi kuwa na Mradi wa Maji na kwamba baada ya Mradi huo kukamilika wananchi wataanza kutumia Maji safi na salama huku wakiondokana na matumizi ya Maji machafu ambayo yaliwasababishia magonjwa ya tumbo na kichocho.

‎Mwisho.

Post a Comment

0 Comments