MHANDISI KUNDO APOKELEWA KWA SHANGWE KATA YA NYANGOKOLWA.

 ‎MBUNGE wa Jimbo la Bariadi Mjini, Mhandisi Kundo Mathew (aliyenyoosha mkono) akiwapungia mkono wananchi ambao hawapo pichani.


‎‎Na Costantine Mathias, Bariadi.
‎

MBUNGE wa Jimbo la Bariadi Mjini, Mhandisi Kundo Mathew amepokelewa kwa Shangwe na Wananchi wa Kata ya Nyangokolwa, Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, kwenye ziara yake ya Kata kwa Kata kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

‎
‎Mhandisi Kundo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, amesema kuwa wananchi wanataka huduma Bora za maji safi na salama na kwamba yeye kama Mwakilishi wao atapaza sauti kuwawakilisha.

‎Wananchi wa Kata ya Nyangokolwa, wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Mbunge wao pamoja na kuwasilisha kero mbalimbali zinazowakabili kwenye maeneo yao.
‎
‎Taarifa zaidi zitaendelea kukufikia.... Hapa SAKAGOI BLOG.







‎

Post a Comment

0 Comments